Zimepita siku nne tuu tangu Taasisi ya dini ya Kiislamu ya Al- Hikma kutangaza nia ya kuwalipia mahari vijana 50 ambao wapo tayari kuoa inaelezwa kuwa zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya nchi wametuma maombi ya kuhitaji ufadhili huo hata kabla ya utaratibu rasmi kutangazwa.
Aidha taasisi hiyo ilitangaza nia ya kuwalipia mahari vijana hao Aprili 9, 2023 jijini Dar es Salaam katika mashindano ya 23 ya Afrika ya kuhifadhi Qur’an kama sehemu ya programu yao ya kuleta manufaa kwa jamii kupitia mashindano hayo.
Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Nurdin Kishki amesema kuwa “ mpaka sasa tumepokea maombi 1000 lakini kama tulivyotangaza muombaji lazima awe muislam sababu ndoa hizo zita simamiwa na Mufti wa Tanzania itakuaje mtu asie kuwa wa dini ya kislamu akafungishwa ndoa ya kiislamu tunaomba tusieleweke vibaya katika hilo” amesema Sheikh Nurdin
Imeeleza kuwa watu hao walituma maombi kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia akaunti ya mitandao mbalimbali ya kijamii ya taasisi hiyo, kupiga simu na hata kutuma ujumbe mfupi wa maandishi.

Leave a Reply