Waliokuwa wakifuga paka 159 waswekwa jela

Waliokuwa wakifuga paka 159 waswekwa jela

Wanandoa kutoka nchini Ufaransa ambao hawajawekwa wazi majina yao wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya tsh 425 milioni baada ya kuwafanyia ukatili wanyama kwa kuwaweka katika mazingira machafu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeeleza kuwa wanyama hao ambao ni paka 159 na mbwa saba walikuwa wakiishi nyumbani kwa wanandoa hao ambapo kufuatiwa na uchunguzi waligundulika kuwa na utapiamlo, upungufu wa maji na magonjwa mengine yaliyotokana na  kuishi katika mazingira machafu.

Aidha ukiachilia mbali hakumu pamoja na faini hiyo wanandoa hao walipigwa marufuku kujihusisha na ufungaji wa wanyama wa aina yoyote.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags