Waliofariki kutokana na kimbunga Freddy wafikia 1000

Waliofariki kutokana na kimbunga Freddy wafikia 1000

Rais kutoka nchini Malawi Lazarus Chakwera ametangaza idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga freddy nchini humo, kuwa imeongezeka na kufikia idadi ya watu 1,000 hali ambayo imeleta tishio kwa raia wa nchi hiyo.

Hata hivyo hakutoa maelezo ni kwanini idadi ya vifo iliongezeka kwa kasi kutoka kwa makadirio ya zaidi ya watu 500 mnamo Machi 20, japokuwa mamia ya watu hawakupatikana hadi kufikia mwishoni mwa mwezi machi.

Aidha kimbunga freddy  kimeathiri zaidi ya watu milioni mbili huku zaidi ya laki tano wakilazimika kuyahama makazi yao kutokana na hofu ya kupoteza maisha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags