Wakili wa Tory kukata rufaa

Wakili wa Tory kukata rufaa

Baada ya ‘rapa’ Tory Lanez kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 siku ya Jumanne baada ya kukutwa na hatia ya mashitaka matatu, Kushambulia Thee Stallion kwa kutumia silaha aina ya Bastola, kubeba bastola isiyo na usajili na kufyatua risasi kwa uzembe.

Wakili wa Tory, Jose Beaz ameonesha kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama dhidi ya kifungo alichotuhumiwa mteja wake.

Wakili huyo amedai kuwa Tory hakupata hukumu ambayo alitarajiwa kuipata adhabu aliyopewa ni kali sana, kwani yeye ni binadamu na atakuwa alifanya tukio hilo kwa bahati mbaya , hivyo kutokana na hayo wanatarajia kukata rufaa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags