Wakili bandia aliyeshinda kesi 26 akamatwa

Wakili bandia aliyeshinda kesi 26 akamatwa

Mamlaka nchini Kenya imemkamata wakili bandia, Brian Mwenda Njagi, ambaye amekuwa akijitangaza kwa uongo kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya.

Chama cha Wanasheria cha Kenya (LSK) tawi la Nairobi Rapid Action Team (RAT) kilimkamata tapeli huyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa umma kuhusu shughuli zake za ulaghai.

Kulingana na chama cha wanasheria nchini Kenya, Njagi si wakili na hana ‘leseni’ ya kutekeleza sheria nchini humo.

Brian licha ya kuwa jaji wa uongo lakini amefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya taarifa zake kujulikana kuwa aliwahi kusimamia kesi 26 na alitoa hoja mbele ya ‘Majaji’ wa Mahakama Kuu, Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Rufani na kushinda kesi zote 26 kabla ya kukamatwa.

Aidha Gavana wa zamani kutoka nchini humo Mike Sonko, amevutiwa na ujasiri wa kijana huyo ambapo kupitia ukurasa wake wa X ameeleza kuwa atajitolea kumsomesha Brian kwenye shule ya sheria ikiwa atakosa pesa ya kwenda kusoma.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags