Wakili amtetea 50 Cent kwa kumjeruhi Mtangazaji na Mic

Wakili amtetea 50 Cent kwa kumjeruhi Mtangazaji na Mic

Baada ya tukio la mwanamuziki 50 Cent kumjeruhi Bryhana Monegain, mtangazaji wa kituo cha Redio cha Power 106, kwenye paji la uso kwa kumrushia microphone usoni, sasa wakili wa 50 Cent aweka utetezi.

Kufuatia tukio hilo lililotokea baada ya 50 Cent akiwa jukwaani akitumbuiza kwenye tour yake ya “Final Lap”  kurusha microphone iliyokuwa haifanyi kazi na ikampata mtangazaji huyo, bidada hakuacha lipite na kuchukua uamuzi kwa kwenda kumshitaki 50 Cent kwa kumjeruhi usoni.

Japo wengi walizungumza tukio hilo kama bahati mbaya, wakili wa msanii huyo anayefahamika kwa jina la Scott Leemon, amefafanua na kuweka wazi wakati akijibu ripoti ya madai hayo kuwa 50 Cent hatawahi kufanya tukio kama hilo kwa makusudi watu waache kupotosha taarifa kuwa alimpiga mtangazaji kwa kukusudia badala yake ni tukio ambalo hakutarajia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags