Wakatoliki kutoa heshima za mwisho katika mwili wa Papa mstaafu Benedict

Wakatoliki kutoa heshima za mwisho katika mwili wa Papa mstaafu Benedict

Waumini wa kanisa Katoliki wataanza leo kutoa heshima zao mjini Vatican kwa papa mstaafu Benedict XVI, ambaye mwili wake utawekwa katika kanisa la Mtakatifu Petro kwa siku tatu kabla ya mazishi yake.

Kiongozi huyo wa kidini Mjerumani, aliyefariki dunia Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95, aliliongoza kanisa katoliki kwa miaka minane kabla ya kuwa papa wa kwanza katika karne sita kujiuzulu mnamo mwaka wa 2013.

Aidha Mrithi wake Papa Francis ataongoza mazishi Alhamisi katika uwanja mkubwa wa Mtume Petro, kabla ya mwili wake kuzikwa katika makaburi yaliyoko chini ya kanisa kuu la Mtume Petro.

Uongozi wa kanisa katoliki mjini Vatican ulitoa jana picha za maiti ya Benedict XVI, akiwa amevalishwa mavazi mekundu ya maombolezo ya upapa na akiwa na kilemba chenye ncha za dhahabu kichwani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags