Waganga wa jadi wapelekwa kigoma

Waganga wa jadi wapelekwa kigoma

Serikali ya kijiji cha Sunukwa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma imeshirikiana na wananchi wa kijiji hicho kwa kuchukua waganga wa jadi zaidi ya 10 kutoka mkoa wa Sumbawanga kwa kusudi la kukaguwa wachawi katka kijiji hicho kutokana na vifo vya kutatanisha hasa kwa vijana vinavyo jitokeza kila leo.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa wilaya ya Uvinza, Dinah Mathamani aliyezuiliwa kuingia kijijini hapo kwa kuwa anapinga mpango wa kuleta waganga hao, amesema

 “Suala tulishalizuia tangu wiki iliyopita, hao wanaojiita waganga wanatakiwa kuondoka katika wilaya yetu atua kali zitachukuliwa dhidi yao na viongozi wanaoshirikiana nao.”alisema mkuu wa wilaya hiyo.

Huku baadhi ya wananchi walikusanyika na kuandamana barabarani wakiimba “Tumechoshwa na uchawi” huku wakiunga mkono mpango huo wa viongozi wao wa kijiji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags