Wafugaji wapigwa marufuku kubeba silaha

Wafugaji wapigwa marufuku kubeba silaha

Rais wa Kenya, William Ruto amesema kuwa wafugaji wa kaskazini hawataruhusiwa tena kubeba silaha wakati wanachunga ng'ombe zao, huku kukiwa na operesheni ya kuwapokonya silaha hizo.

Gazeti la Daily Nation lilimnukuu Rais huyo, "Kuanzia sasa, hakuna mtu atakayeruhusiwa kuchunga akiwa na silaha. Silaha ni za maafisa wa usalama tu."

Msamaha wa kusalimisha bunduki kwa hiari kaskazini mwa nchi hiyo ulikwisha tarehe 21 Februari, huku bunduki 19 pekee ndizo zilizopatikana. Serikali inakadiria kuwa maelfu ya silaha zinashikiliwa na raia.

Aidha, Ruto aliongozea kwa kusema kuwa serikali itawekeza $156.4m kununua vifaa vya kupambana na ugaidi na uhalifu mwingine.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags