Wafanyakazi Watakaoanzisha Mahusiano Kupewa Pesa

Wafanyakazi Watakaoanzisha Mahusiano Kupewa Pesa

Baadhi ya kampuni kutoka nchini China zimeripotiwa kuwa na mpango wa kuhamasisha wafanyakazi wasio na wapenzi kwa kuwapa pesa.

Imeelezwa kuwa wafanyakazi wasiokuwa na wenza watatakiwa kuanzisha uhusiano na wafanyakazi wenzao ambapo kila mmoja wao atakabidhiwa dola 10 kila mwezi.

Aidha wafanyakazi hao watakaoanzisha uhusiano watatakiwa kujitambulisha rasmi katika jukwaa lililoandaliwa ndani ya kampuni huku wakipewa pesa za ziada dola 140 endapo watadumu kwa miezi mitatu bila kuachana.

Aidha inadaiwa kuwa mpango huo umeanzishwa ili kuongeza hisia za mshikamano na furaha kwa wafanyakazi katika kipindi hichi ambacho nchi hiyo imekumbwa na viwango vidogo vya ndoa na uzazi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags