Wafanyakazi Kenya watakiwa kutoa 3% kuchangia Taifa

Wafanyakazi Kenya watakiwa kutoa 3% kuchangia Taifa

Rais William Ruto amesema wananchi wote nchini humo wanao wafanyakazi serikalini kuanzia sasa watakuwa wakichangia asilimia 3 ya mapato yao kwenye mfuko wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu ili kuwasaidia watu wengi zaidi kununua na kumiliki nyumba hizo.

Kifuatia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari ameeleza kuwa "Kila mfanyakazi anatakiwa kuchangia asilimia 3 Sheria itamlazimisha mwajiri wao pia kuchangia asilimia 3 kwenye mfuko huo "alisema Rais Ruto

Aidha Ruto amesema wakati Serikali inapoanzisha mpango huo wa ujenzi lazima kuwe na mpango madhubuti unaolenga kushughulikia ufadhili wa watu wenye kipato cha chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags