Vitu usivyovijua ambavyo Simu yako inaweza kuvifanya

Vitu usivyovijua ambavyo Simu yako inaweza kuvifanya

Watu wengi wamekuwa wakitumia simu kuwasiliana na ndugu zao mbalimbali kwa kuwapigia au kuwatumia ujumbe mfupi wa maneno maarufu kama sms.

Lakini nataka nikujuze kwamba mbali na kuandika ujumbe wa WhatsApp, kupiga simu kuangalia mtandao wa facebook na Instagram kuona kile rafiki zako walichochapisha, simu yako janja inaweza kukusaidia zaidi.

Leo kwenye listi tumekusogezea mambo sita ambayo simu yako inaweza kuyafanya ambayo najua uwenda ulikuwa unayajua na wewe ambaye ulikuwa huyajui leo nakujuza.

  1. Unaweza kupiga picha huku ukirekodi kanda za video

Upigaji picha wa simu umekuwa jambo la kila siku kutokana na uwepo wa mtandao na mitandao ya kijamii. Kila siku mamilioni ya raia huchukua na hata kusambaza picha kwa kutumia simu zao za janja.

Lakini je unajua kwamba unaweza kupiga picha wakati unapoendelea kurekodi kanda ya video? Ndio unaweza kwa kutumia simu aina ya Adroid pamoja na ile ya iPhone.

Jinsi ya kufanya jambo hilo, kwanza gusa skrini yako unaporekodi video, iwapo una simu aina ya iPhone unatakiwa kubonyeza mahali unapotumia kupiga picha, kitufe cheupe karibu na kitufe cha kurekodi video.

Iwapo una iPhone bonyeza na kuzuia kitufe cheupe kushoto mwa kitufe chekundu cha kurekodia unaporekodi

Hatahivyo hali ya picha hizo haiwezi kuwa nzuri ukilinganisha na ile ambayo unapeta iwapo ungekuwa unapiga picha ya kawaida , lakini ni njia mojawapo ya kupiga picha kitu kinachofanyika wakati huo.

  1. Unaweza kusoma ujumbe wako na emoji

Je umechoka kutazama skrini ya simu yako mara kwa mara?

Unaweza kutumia simu yako kusoma ujumbe unaopokea kana kwamba unasikiza redio.

Cha kufanya, sema neno hili kwa simu yako: Siri- au Google iwapo unatumia simu aina ya Adroid- soma ujumbe wangu.

Halafu unaweza kuamua iwapo utazijibu ama iwapo unataka simu yako aina ya smartphone kurudia tena ujumbe huo.

Ujanja huo sio tu kwa ujumbe wa SMS: Pia unaweza kuutumia kwa WhatsApp.

Je wajua kwamba simu yako inaweza kusoma emoji?

Iwapo una simu aina ya Apple, ambia Siri. ''Siri nisomeee ujumbe mpya wa WhatsApp''. Itausoma mara moja. Pia itakwambia ni nani aliyetuma na ni wakati gani uliwasili. lakini la kufurahisha ni vile inavyosoma emoji. jaribu!.

Iwapo unatumia simu aina ya Adroid, ni sharti utumie programu fulani. Programu hizo ni Hatomic ama ReadItToMe

  1. Wazuie wengine kutotumia programu ya simu yako

Iwapo utamsaidia rafiki yako kwa kumpatia simu yako lakini hutaki afungue programu zako ama kusoma ujumbe wako wa WhatsApp unaweza kubadili programu zako na kumzuia na kutoweza kuingia bila kutumia neno la siri.

Unaweza kutumia programu mbadala kwa jina 'Guided Aces's katika setting na baadaye nenda kwa accesibility na kubonyeza kitufe cha programu hiyo unayotaka kubadilisha.

Iwapo ni Android utaipata katika location na security. Unaweza kuzuia matumizi ya programu nyengine

Pia unaweza kutumia programu kama vile Applock ambayo pia inazuia mtu kuingia katika programu ya Google play ili asiweze kupakua programu bila wewe kujua.

Programu nyengine mbadala ni ile ya Hexlock ambayo inakuwezesha kutengeneza 'profile' tofauti za watu na imeelezewa iwapo unataka kuwaachia watoto simu yako.

Iwapo una simu aina ya Iphone, tumia programu ya Notes.

Katika kitufe cha alama ya ongeza tumia Scan documents. Hatua nyengine unazofaa kuchukua ziko sawa kama zile zinazotumika na Google drive, mwisho bonyeza kitufe cha hifadhi ama save.

  1. Kusawazisha

Iwapo unataka kuweka boksi katika eneo tambarare lenye usawa unaweza kutumia simu yako

Katika iOs kuna kitufe mbadala kilichojificha kwa jina Measure program kipimo cha kusawazisha kipo ndani ya simu yako ya iphone

  1. Kutambua vyuma

Iwapo umepoteza pete yako ama vipuli vyako vya dhahabu na huwezi kuvipata simu yako inaweza kuwa kifaa muhimu sana

Kwa wale wanaotumia simu aina ya Android, kuna programu inayotoa fursa hiyo kwa jina Metal Detector.

Ni bure na inatumia sensa ya sumaku ya simu yako.

Matumizi yake ni rahisi sana: Fungua programu hiyo , peleka simu hiyo mahali unapotafuta kifaa hicho cha chuma , iwapo una bahati simu hiyo itapiga king'ora.

je umepoteza pete yako?, tumia simu yako kuitafuta

  1. Kuskani Nyaraka

Iwapo una nyaraka ambayo unahitaji kwenda katika tarakilishi lakini hauna skana, unaweza kutumia simu yako ya rununu.

Kupitia programu kama vile Genius scan, Cam Scanner na Office Lens unaweza kubadilisha nyaraka yoyote kidijali kwa sekunde chache.

Unaweza kufungua programu ya Google Drive katika simu aina ya Android ambayo iko huru -ongeza kitufe (the + symbol) chagua kitufe kilichoandikwa "Scanning" ili kuamsha kamera ya simu yako.

Unapoipima vizuri na kuhakikisha kuwa nyaraka zote zipo ndani ya skrini chukua nyaraka hizo na kuweka ndani ya picha. Kwa kubonyeza kitufe cha Accept picha hiyo itahifadhiwa katika PDF.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa BBC.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags