Video ya mtoto mwenye ngozi nyeusi kunyimwa medali, Simone apiga vita ubaguzi wa rangi

Video ya mtoto mwenye ngozi nyeusi kunyimwa medali, Simone apiga vita ubaguzi wa rangi

Kama ilivyo kawaida ya teknolojia kutunza vitu na kuviibua upya ndiyo video ya mtoto mwenye ngozi nyeusi ya mwaka 2021 nchini Ireland imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikihusisha Shirika la Mchezo wa viungo kutajwa kuhusika na ubaguzi wa rangi baada ya video hiyo kuonesha mtoto mwenye ngozi nyeusi aliyeshiriki mashindano hayo akinyimwa medali huku wenzake wenye ngozi nyeupe wote wakipewa medali hizo.

Aidha bingwa wa Olimpiki Simone Biles amelaani tukio hilo na kusema aliamua ku-post video hiyo ili kumuunga mkono mtoto huyo baada ya wazazi wake kumueleza walivyoumizwa na kitendo hicho mwanamichezo huyo alisema kuwa hakuna nafasi ya ubaguzi wa rangi katika mchezo wowote.

 licha ya shirika hilo la michezo kuomba radhi kwa umma kwa tukio hilo, baada ya wazazi wa msichna huyo kusema kuwa kitendo hicho ni ubaguzi wa rangi.
.
.
.
ili uweze kuangalia video hii pitia kwenye Instagram ya @mwananchiscoop
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags