Vazi la kuzingatia katika mtoko wa kwanza na mpenzi wako (first date)

Vazi la kuzingatia katika mtoko wa kwanza na mpenzi wako (first date)

Na Habiba Mohammed

Whats goooood, whats goooooood my beautiful people!!… It’s another furahiiiiii day kwenye kona yetu ya Fashion ndani ya Mwananchi Scoop. Ebwaaana leo sina mambo mengi sana kubwa zaidiii kuwekana sawa katika mavazi katika mitoko yetu.

Ebwaana mapenzi hunogeshwa na mitoko ya hapa na pale. Leo nakupa maujanja, mambo ya kuzingatia katika mavazi kwenye mtoko wako wa kwanza na mpenzi wako (first date).

MAMBO YA KUZINGATIA

-Fahamu rangi unazozipenda na kukupendeza

Hapa unatakiwa kukumbuka maongezi yenu ya awali ulipoulizwa “unapenda rangi gani,” ili kujua mpenzi wako anapenda rangi kulingana na nguo ulizonazo.

Kwa mwanamke inapendeza kuvaa nguo yenye rangi inayoendana na ngozi yako kwa kuzingatia rangi baadhi ya maeneo yako katika mwili kama magoti, mikono na miguu, vilevile katika rangi ulizonazo unatakiwa kuzingatia hali ya hewa kwa mfano rangi nyeusi na jua kalii inaweza kukusababishia jasho pia rangi nyeupe kwenye mvua rahisi kupata matope hivyo basi itakusaidia kuepuka kasoro ndogo ndogo.

-Fahamu sehemu unayoenda kukutana na mpenzi wako

Muhimu kufahamu sehemu unayoenda kukutana na mpenzi wako hii itakusaidia kujua aina ya nguo utakayovaa pia viatu, mfano kama sehemu  mnayoenda kukutana ni ufukweni matembezini utatakiwa kuvaa viatu vya kawaida na sio kuvaa “high heels” ila unaweza kuvaa “high heels” kulingana na eneo mnaloenda kukutana na kuwa na amani na aina ya kiatu ulichovaa ili uweze kufurahi na mpenzi wako.

-Kuwa halisi

Ni sahihi kujiremba au kuvaa mavazi mazuri kwa ajili ya kumvutia mpenzi wako na kujiona wa pekee mbele yake, unachotakiwa kuepuka kujiremba sana kiasi cha kupoteza uhalisia wako, hii itasaidia mpenzi wako kukupenda kwa jinsi ulivyo pia itakusaidia hata ikitokea umekosa hivyo vipodozi utabaki kuwa yuleyule ambaye mpenzi wako amekuzoea.

-Shirikisha rafiki juu ya muonekano wako

Baada ya kuchagua nguo unazotaka kuvaa inafaa pia kushirikisha rafiki au watu wako wa karibu juu ya muonekano ulionao. Hii itasaidia kuboresha zaidi muonekano wako kwa kuongeza au kupunguza baadhi ya vitu katika muonekano wako kwa mfano kupunguza vipodozi make-up) itasaidia kukufanya uwe na amani kwenye mtoko wako na mpenzi wako.

-Chagua sehemu unapopaweza kifedha

Mtoko ni mtoko tu na lengo la mtoko ni kufurahi na mpenzi wako na kupiga stori vilevile kupiga picha nzuri kuweka kumbukumbu baina yenu, unatakiwa kuchagua eneo unaloliweza kumudu kifedha hii itakusaidia kuwa mkarimu kwa mpenzi wako kwa kutumia kilichopo kwenye bajeti ya fedha uliyonayo,kuwa na Amani na kufurahia mazungumzo.

Hayoo ndo mambo muhimu ya kuzingatia kwa mara ya kwanza kwenda kukutana na mpenzi wako, mwanzo wa mtoko wa kwanza, mingine hufata ila kuna wale wachumba au wapenzi huwa hawasemii ulipokosea utajikuta tu hakuna “Babe leo tutoke’’ na hujui shida nini, kikubwa kuzingatia  ili mambo yawe pouwah.

Dondosha comment yako ukitueleza mtoko wako wa kwanza na mpenzi wako ulivaa je? Je simu za mitoko bado zinaitaa au ndo hayatuhusu? hahaha till next time.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags