Vanessa, Rotimi watarajia mtoto wa kiume

Vanessa, Rotimi watarajia mtoto wa kiume

 

Moja kati ya story iliyobamba katika mitandao ya kijamii kwa siku ya jana na leo ni ya mwimbaji Staa kutoka Tanzania anayeishi Atlanta Marekani Vanessa Mdee.

Vanessa jana alitoa picha zake ambazo ni exclusive kutoka jarida la People zilizomuonesha kuwa ni mjamzito huku akiziambatanisha na caption mbalimbali.

Katika picha hizo Vanessa alionekana na mpenzi wake Rotimi na kuandika “The greatest gift of all, thank you Jesus for choosing us, it is a true true honor. We are overjoyed

Isaiah 55:2-All your children shall be taught by the lord, and great shall be the peace of your children,” ameandika Vanessa

Naye Rotimi aliandika ““Naomba mtoto wetu awe na moyo wako, akili, na imani yako, ninaahidi kukulinda wewe na mtoto wetu kwa kila nilichonacho,” ameeleza

Hata hivyo Vanessa ameweka wazi yeye na mpenzi wake Rotimi wanatajaia kupata mtoto wa kiume hivi karibuni.

Mahusaiano ya Vanessa na Rotimi waliwekwa wazi mwaka 2019 ikiwa ni miezi michache tangu aachane na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu msanii wa bongo fleva, Juma Jux.

Licha ya nyakati tofauti kuwepo kwa tetesi za kuwa mjamzito, Vanessa alikanusha hilo na kuwalaumu wale wote waliokuwa wakisema jambo hilo ambalo alidai linamfanya mama yake mzazi kupaniki.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags