Vanessa Mdee atamani mtoto wa pili

Vanessa Mdee atamani mtoto wa pili

Msanii wa muziki nchini Tanzania ambaye kwa sasa anaishi huko Marekani, Vanessa Mdee ameweka wazi kuwa anatamani kuongeza mtoto wa pili siku za hivi karibuni.

Hiyo imekuja baada ya kuposti video katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha baba wa mtoto wake wa kwanza Rotimi akiwa na mtoto huyo na kuandika ujumbe ambao umeonesha wazi matamanio ya Vanessa ya mtoto wa pili.

Vanessa katika posti hiyo ameandika jinsi gani wawili hao wanavyompenda mtoto wao na kumalizia na ‘baby number two loading’ ikimaanisha mtoto wa pili yupo njiani.

“When I tell you these two melt my heart I walk in on them having Daddy-Son-Fun, baby number two loading,” aliandika Vanessa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags