Valentine Korea Wanawake ndiyo wanawapa Wanaume zawadi

Valentine Korea Wanawake ndiyo wanawapa Wanaume zawadi

Inawezekana ikawa ni ajabu lakini huo ndiyo utaratibu ulioko nchini Korea Kusini ambapo ikifika Februari 14, siku ya Valentine, wanawake ndio wanawapa wanaume zawadi tofauti na nchi nyengine ambazo wanawake ndiyo mara nyingi wanapokea zawadi kutoka kwa wanaume.

Kwa mujibu wa tovuti ya #90dayKorean, inaelezwa kuwa zawadi hizo mara nyingi huwa ni maua yenye rangi nyekundu au chocolate na baada ya Valentine huwa kuna sikukuu nyengine ya wapendanao iitwayo ‘White Day’ inayofanyika Machi 14, ambapo wanaume ndiyo hutoa zawadi.

Zawadi hizo huwa ni sehemu ya kujibu kile ambacho wamefanyiwa na wapenzi wao kwenye Valentine na mara nyingi huwa wanatoa maua au vitu vyenye rangi nyeupe.

Mbali sikukuu hizi mbili tovuti ya #PermataBank inafichua kwamba huwa kuna sikukuu nyengine nyingi zinazohusu mahusiano nchini humo kama ‘Black Day’ inayosheherekewa April 14, na wale ambao wapo single.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post