Kwa mujibu wa utafiti kutoka kwa ‘Plos One’ umebaini kuwa njaa inaweza kumfanya binadamu kuchukua maamuzi magumu.
Utafiti huo pia ulionesha kwamba njaa haichochei tu hasira na kukasirika, lakini pia inaathiri jinsi mtu anavyofikiria na kutafsiri vibaya mambo yanayoendelea ulimwenguni.
Mtu unapokuwa na njaa uwezo wa kufikiri unakuwa mdogo na kumfanya mtu huyo aweze kutafsiri mambo kwa njia hasi na kuchukua hatua haraka.
Hivyo basi katika kuhitimisha utafiti huo watafiti wanabaini kuwa mahitaji muhimu ya binadamu yanaweza kuathiri saikolojia ya mtu.
Tuambie ni maamuzi gani magumu huwa unayachukua pale unapokuwa na njaa?
Leave a Reply