Utafiti: Kumchunga sana mtoto kunampunguzia muda wa kuishi

Utafiti: Kumchunga sana mtoto kunampunguzia muda wa kuishi

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Shirikisho cha São Carlos na Chuo Kikuu cha London, kwa watu 1,000 waliozaliwa katika miaka ya 1950 na 1960, umegungua kuwa tabia ya wazazi kuwachunga watoto wao kupita kiasi huwapunguzia miaka ya kuishi.

Utafiti huo umegundua kuwa wanaume ambao enzi za utoto wao walikuwa wanalindwa kupita kiasi na kupewa uhuru mdogo kutoka kwa baba zao wapo katika hatari ya 12% kufariki mapema kabla ya kufikisha umri wa miaka 80.

Kwa upande wa wanawake hatari ya kufariki kabla ya kufika umri wa miaka 80 inaongezeka kwa 22%, huku kwa upande mwingine wanawake ambao walitunzwa vizuri na mama zao wakati wa utoto, hatari inaweza kupungua kwa 14%.

Utafiti huo pia umeenda mbali na unaonesha kuwa wanaume ambao waliishi na mzazi mmoja tu utotoni wapo kwenye hatari kubwa ya 179% kufariki kabla ya kufikisha miaka 80.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags