Utafiti: Kula ngozi ya kuku ni hatari

Utafiti: Kula ngozi ya kuku ni hatari

Inaripotiwa kuwa ngozi ya kuku inakiwango kikubwa cha mafuta ambayo ni hatari kwa afya ya binaadamu.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali duniani zinaeleza kuwa ngozi ya kuku ina mafuta mengi, kwa hivyo watu wengi huiondoa ili kuokoa kalori, licha ya kuwa inasaidia kuweka unyevu kwenye nyama wakati wa kupika kwenye oveni au grill.

Mtaalamu wa lishe kutoka ‘Meat Nutrition Information Center’ nchini Marekani, María Dolores Fernández Pazos, amethibitisha kuwa ngozi ya kuku ina asilimia 32 ya mafuta.

Pia mtaalamu huyo ameeleza kuwa kati ya mafuta haya yaliyomo kwenye ngozi ya kuku theluthi moja ni mafuta yasiyo na madhara ambayo husaidia kuboresha viwango vya damu na theluthi mbili ya mafuta ndiyo ambayo huchangia kuongeza viwango vya mafuta yasiyofaa katika mwili wa binadamu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post