Usingizi wa mchana ni mzuri kwa ubongo wako

Usingizi wa mchana ni mzuri kwa ubongo wako

Watafiti kutoka chuo Kikuu cha London wanaeleza kuwa kupata muda wa kulala kidogo mara kwa mara ni vizuri kwa ubongo wetu na husaidia kuuweka ubongo kuwa mkubwa kwa muda mrefu.

Watafiti hao wamebaini kuwa ubongo wa watu wanaopata muda kidogo wa kualala ulikuwa na sentimita za ujazo wa 15 sawa na inchi 0.9 na hali hiyo pia inachelewesha kuzeeka kwa kati ya miaka mitatu na sita. Lakini, wanasayansi wanapendekeza kulala kwa chini ya nusu saa.

Wameongeza kuwa kwa wale wanaofanya kazi mchana, usingizi wao ni wa nadra sana kutokana na kubanwa na kazi nyingi, huku utamaduni wa kufanya kazi mara nyingi ukipinga suala zima la kulala mchana maeneo ya kazini.

“Tunapendekeza kwamba kila mtu anaweza kupata faida fulani kutokana na kulala”Daktari Victoria Garfield anasema.

Kulala usingizi kumeonekana kuwa muhimu kwa maendeleo ya ukuaji hasa kipindi cha utoto, na hali hiyo hupungua kwa kasi kubwa kwenye utu uzima sana kisha kupata umaarufu tena baada ya kustaafu, huku asilimia 27 ya watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65 wakiripoti kupata usingizi wakati wa mchana.

Daktari Garfield anasema ushauri wa kulala usingizi ni jambo rahisi sana kwa kulinganisha na kupunguza uzito au mazoezi ambayo ni kazi ngumu na hatua kubwa kwa watu wengi.

Ubongo kwa kawaida hupungua kwa umri, lakini ikiwa unapata usingizi unaweza kusaidia kuzuia magonjwa kama vile Alzheimers tatizo linalomfanya mtu kutoshiriki katika mazungumzo kwa muda mrefu, japo utafiti zaidi bado unahitajika.

Kwa ujumla afya ya ubongo ni muhimu kwa ajili ya kukulinda dhidi ya shida ya akili na hali hiyo inahusishwa na usingizi usio na wasiwasi.

Watafiti wanapendekeza kuwa tabia ya kutolala kwa wakati kunaathiri afya ya ubongo kwa kuathiri miunganisho kati ya seli za ubongo.

“Kwa hivyo, kulala mara kwa mara kunaweza kusaidia kukulinda dhidi ya kuzorota kwa mfumo wa neva kwa kufidia usingizi duni” mtafiti Valentina Paz alisema.

Hata hivyo, Daktari Garfield huwa hapendi sana kutafuta eneo zuri la kukalala mchana akiwa kazini lakini badala yake huwa anatumia njia mbadala za kutunza ubongo wake.

“Kusema kweli, ningependa kutumia dakika 30 kufanya mazoezi kuliko kulala, labda nitajaribu na kupendekeza kwamba mama yangu afanye hivyo”

Chanzo BBC

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags