Usimaindi maana itakugusa tu

Usimaindi maana itakugusa tu

Ukiichunguza jamii yetu. Utabaini matajiri wengi ni wenye elimu kiasi. Au hawakusoma. Wasomi wengi wana 'laifu' ya kawaida na huishia kujenga na gari ya kutembelea tena ya mkopo!

Kwa lugha 'staarabu' tuseme wengi wanaungaunga. Matajiri wachache sana walisoma sana. Na hili jambo huanzia shule, vyuoni wanakopatia usomi wao. Hujengwa katika 'laifu' la ubinafsi.

Huaminishwa kwamba ukupatia maswali yote ndo ufaulu. Ukikosea ni mjinga, umefeli. Na wakati katika ya michakato wa kutafuta, kujaribu na kukosea ni sehemu ya ufaulu.

Wasomi wengi huogopa kukosea na hawapendi kujaribu 'madili'. Kwa hofu ya kushindwa na huamua kufa kilofa. Wengi hutegemea 'salare' pekee bila kujiongeza.

'Klasi' kuna ubinafsi na siyo umoja. Mfano 'pepa' kila denti hujifanyia 'pepa' kivyake. Mkisaidiana ndani ya chumba cha 'pepa' ni kosa na adhabu ni kali ikiwemo kufutiwa na mtihani.

Katika maisha ya utafutaji, unahitaji ushirikiano mkubwa. Baina yako na wadau, wateja, 'stafu' au marafiki. Huwezi kupaa kiuchumi ukiwa na 'mentalite' ya ubinafsi inayoongoza darasani!

Simaanishi elimu haina maana, ni kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii. Lakini usibebe kile unacholishwa 'klasi' ukaleta na huku mitaa. Utakufa masikini na vyeti vyako.

Mtaa ni kusapotiana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags