Urusi kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja

Urusi kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja

Urusi inatarajia kupitisha muswada wa marufuku dhidi ya kueneza kile kinachoitwa "propaganda za wapenzi wa jinsia moja" kwa watu wote.

Sheria itaruhusu taarifa yoyote kwenye mtandao inayojadili mada za LGBT kuzuiwa na filamu zinazo hamasisha wapenzi wa jinsia moja kupigwa marufuku.

Sheria hiyo imeboreshwa kupitia sheria iliyopo ya 2013, ambayo inafanya kutoa taarifa kuhusu wapenzi wa jinsia moja kwa watoto kuwa kosa la jinai.

Faini ya kati ya rubles 50,000 (£705; $815) na rubles 400,000 itatozwa, huku wasio Warusi wanaokiuka marufuku hiyo watakabiliwa na kufukuzwa nchini.

Uidhinishaji wa awali wa kuitumia sheria hiyo ulipigiwa kura na Jimbo la Urusi Duma kwa kauli moja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post