Urembo si sura na mavazi tu, hata mwonekano wa jiko lako

Urembo si sura na mavazi tu, hata mwonekano wa jiko lako

Habari msomaji wetu ni siku nyingine tena tunakutaka ili  kujuzana mambo mbalimbali kuhusiana  masuala ya urembo, mitindo na mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujua zaidi.

Lakini leo nitakuwa tofauti kidogo kwani napenda kukujuza juu ya mambo muhimu ya kupendezesha jiko lako na kufanya liwe na mwonekano wa kuvutia.

Mwanamke mwenzangu leo nakujuza kuwa urembo si sura na mavazi tu katika mwili wako hata mwonekano wa jiko lako nyumbani.

Mara nyingi watu wanapoongelea kupamba nyumba wanazingatia zaidi sebule na sehemu zingine zinazoonekana lakini wanasahau kabisa jiko.

Jamani jikoni pia linatakiwa kupendeza ili kumpa mpishi hamu ya kupika chakula kizuri na kitamu ili mlaji naye apate hamu kubwa ya kula chakula hiko.

Ieleweke kuwa mlaji huyo atapata hamu ya kula chakula hicho kama tu kitakuwa kimepikwa katika mzingira safi na mazuri, Kwa upande mwingine hata wewe mpishi unapata nguvu ya kuwepo jikoni endapo utaweka jiko lako katika mazingira mazuri ya usafi.

Wanawake wengi katika nyumba zao wamekuwa hawapambi na kutengeneza jiko kwa madai ya kuwa gharama ni kubwa ya kufanya maboresho ukizingatia kuwa wageni wengi hawafikagi jikoni.

 

Ukweli ni kwamba hiki ni kisingizio kisichofaa hata kidogo kwani kupamba au kutengeneza jiko zuri si lazima utumie gharama kubwa hata kuweka mpangilio mzuri wa jiko ni urembo tosha.

Yafuatayo ni mambo madogo ambayo unaweza kufanya ili kupendezesha jiko lako na kulipa mvuto wa kupendeza.

Kwanza Mpangilo wa vitu, ili jiko livutie ni lazima liwe na mpangilio mzuri na wenye nafasi kupanga huku kunahusisha meza ya jiko, vyombo kabatini, majiko, friji na kila kitu kikaacho jikoni.

Jitahidi vyombo vyote vikae ndani ya kabati la vyombo na kama kabati ni dogo na vyombo ni vingi basi tunza ndani ya boski au mabeseni makubwa ili mradi tu visisambae jikoni.

Pili matumizi ya rangi zinazong’ara, Rangi zinazongara hupendezesha sana jiko ni vyema kununua vitu vyenye rangi za kung’ara ili kung’arisha zaidi jiko, Rangi hizo ni kama kijani, njano, nyekundu, bluu, nyeupe, orenji na zingine.

Tatu, kuweka urembo wa aina mbalimbali, ni vyema kuwa mbunifu na kutumia urembo wa aina mbalimbali kupendezesha jiko. Unaweza tumia vyungu  vyenye rangi tofauti tofauti za kuvutia na kuvipanga juu ya kabati au sehemu nyingine yoyote unayoona inafaa.

Nne, nunua vyombo vizuri, Ni ukweli usiopingika kuwa vyombo vizuri hulipa jiko mvuto na muonekano wa kuvutia, nunua vyombo vyenye maumbo na rangi mbalimbali mfano badala ya kununua sahani za duara kila mara unaweza nunua sahani za pembe nne au zenye umbo la yai.

Tano, ondoa vitu usivyotumia, Ni vyema ukaondoa jikoni vitu usivyotumia kwani vinachukua nafasi na kujaza jiko bila sababu za msingi, watu wengi hupenda kutunza vitu visivyotumia kama majiko mabovu, vyombo vibovu na kadhalika.

Tabia hiyo ni mwanzo wa uchafu jikoni hivyo kusababisha uwepo wa mende na panya lakini pia umfanya mgtu asinunue vitu vipya kwa kujipa moyo kua anavyo wakati ukweli ni kwamba alivyonavyo ni vibovi na havifai.

Ni muhimu kama wanawake kuzingatia haya mambo kwani nawaambia ukiyafanya utafurahi kuingia jikoni kwako kila wakati na kupika chakula kizuri na kitamu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags