Urafiki wa Davido na Chris Brown umekolea nazi

Urafiki wa Davido na Chris Brown umekolea nazi

Urafiki wa wanamuziki Davido na Chris Brown, unaonekana kukolea nazi kila kukicha. Hivi sasa Davido atoa shukrani kwa Chris baada ya mkali huyo kutoka Marekani kumpatia zawadi ya cheni.

Cheni hiyo ya thamani aliyozawadia Davido na Chris, ina kidani kilichoandikwa (OHB) likiwa na maana ya 'Original Hood Bosses', neno ambalo wawili hao wamelichora tatoo kwenye miili yao.

Chris kwa upande wake ana tatoo shingoni iliyoandikwa neno hilo huku kwa upande wa Davido amechora kwenye mkono wake wa kulia. OHB inahusisha watu maarufu ambao wana ukaribu na Chris, kati yao akiwemo Tyga, Kevin Gates, Young Thug,Tyga.

Ikumbukwe kuwa urafiki wa Chris na Davido unaonekana kushika kasi kila kukicha tangu wawili hao wafanye ngoma ya pamoja iitwayo 'Blow My Mind' iliyotoka miaka minne iliyopita.

Hata hivyo miezi michache iliyopita Davido amesikika kwenye ngoma ya Chris iitwayo 'Sensational' ambayo video yake imeachiwa miezi mitatu iliyopita. Licha ya hayo wawili hao pia wameonekana kupeana 'sapoti' kwenye kazi zao kama vile kupandishana jukwaani na kushirikiana kwenye kusukuma ngoma zao, kama alivyofanya Chris kwenye 'Un Available' ya Davido.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags