Unyoya mmoja wa ndege aina ya Huia kutoka New Zealand umeripotiwa kuuzwa kwa dola 28,417 ikiwa ni zaidi ya Sh 73 milioni katika mnada wa Webb.
Kwa mujibu wa tovuti ya #Cnn imeeleza kuwa mara ya mwisho kuonekana kwa ndege huyo ni mwaka 1907 lakini bado unyoya wake unamng’ao wa kipekee.
Unyoya huo ambao ulitakiwa kugharimu dola 3,000 bado unatajwa kuwa ndiyo unyonya uliyovunja rekodi kwa kuuzwa bei ghali zaidi.
Ndege aina ya Huia walikuwa watakatifu kwa watu wa jimbo la Maori ambapo manyoya yao mara nyingi yalitumika kuvaliwa kichwani na machifu pamoja na familia zao.
Leave a Reply