Unyanyasaji wa kijinsia vyuoni na jinsi ya kukabiliana nao

Unyanyasaji wa kijinsia vyuoni na jinsi ya kukabiliana nao

Kuna wakati unakutana na changamoto ya kunyanyaswa kijinsia na usiwe na uelewa kwamba kitendo ulichofanyiwa ni unyanyasaji lakini kwa sababu ya ukosefu wa uelewa juu ya elimu ya unyanyasaji mtu anaweza kuhisi kwamba kilichotokea either ni sawa au sio sawa lakini ukashindwa kutoa taarifa popote kwa kuhofia kuchekwa, kuaibika au kudharaulika.

Unyanyasaji wa kijinsia ni tatizo linalojitokeza katika maeneo mengi duniani, na vyuo vikuu havijanusurika na tatizo hili. Wanavyuo wanakutana na changamoto kubwa za kijinsia ambazo zinaweza kudhoofisha uwezo wao wa kusoma, kustawi, na kufurahia maisha yao ya vyuo vikuu. Leo tutaangaazia njia kadhaa za namna unyanyasaji wa kijinsia unaweza kujitokeza na nini kifanyike kukabiliana na unyanyasaji huo kwa wanavyuo.

Unyanyasaji wa kijinsia wa kimwili, ni pamoja na vitendo vya kimwili vya unyanyasaji kama vile kuguswa bila ridhaa au ngono kwa nguvu. Wanafunzi wakike na wakiume wanaweza kuwa wahanga wa unyanyasaji wa kimwili wa namna hii wanapokua vyuoni.

Unyanyasaji wa kijinsia wa kisaikolojia, mara nyingi, unyanyasaji huu hufanyika kupitia maneno au vitendo vinavyowatia wanavyuo katika hali ya unyonge au kuwafanya wahisi hawana thamani. Hali kama hii inaweza kujumuisha kuitwa majina ya kashfa au kutumia lugha ya matusi.

Unyanyasaji wa kijinsia wa kifikra, hapa, wanavyuo wanaweza kudhalilishwa kifikra kuhusu jinsia zao. Mara nyingine, wanafunzi wanaweza kuhisi kuwa hawapati fursa sawa za kielimu au kazi kwa sababu ya jinsia zao.

Unyanyasaji wa kijinsia wa kimfumo, miundo ya kijamii au kimfumo nayo kwa upande mmoja inaweza kudhoofisha wanavyuo kulingana na jinsia zao. Kwa mfano, mfumo wa kielimu au wa kazi unaweza kuwa na ubaguzi wa kijinsia ambao unazuia maendeleo ya wanafunzi wa kike au wa kiume.

Changamoto hizi za unyanyasaji wa kijinsia vyuo vikuu zinaweza kuathiri sana uwezo wa wanavyuo kufanikiwa katika masomo yao na baadhi kushindwa kutimiza ndoto zao pia inaweza kupelekea.

Kupoteza kujiamini, wanavyuo wanaokumbwa na unyanyasaji wa kijinsia wanaweza kupoteza confidence zao na uchangamfu kama walivyokua awali. wanaweza kuanza kuamini kuwa hawastahili kufanikiwa au kuhisi kuwa wao ndiyo wanaokosea.

Pia kuna uwezekano wa kupata athari za kisaikolojia kama vile wasiwasi, unyogovu, au hata mshituko wa baada ya unyanyasaji.

Kushuka kwa ufaulu wa mwanafunzi darasani pia kunaweza kuwakumba wanavyuo wanaokutana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia hivyo kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao kwa sababu ya kuathiriwa na hali hiyo.

Kuna namna nyingi za kupambana na unyanyasaji wa kijinsia tunapokua vyuoni baadhi yake ni,

 

Kwanza kabisa kutoa Elimu juu ya unyanyasaji wa kijinsia ni mojawapo ya njia inayoweza kuwapa wanavyuo maarifa na ufahamu wa tatizo hili na jinsi ya kujilinda.

Pia wanafunzi wanaokumbwa na unyanyasaji wanapaswa kutengeneza mazingira rafiki ya kuwa na urahisi kwa upatikanaji wa huduma za kisaikolojia ili kusaidia katika kushughulikia athari za kisaikolojia zinazokua zimejitokeza kama athari ya kunyanyaswa.

Vyuo vikuu vinaweza kuweka mifumo ya kusikiliza na kushughulikia malalamiko ya unyanyasaji wa kijinsia ili wahanga waweze kuripoti matukio na hatua zichukuliwe kwa haraka kwa washtakiwa wa vitendo hivyo vya unyanyasaji.

Vilevile unapohisi kwamba rafiki au mwanachuo mwenzako anapitia au amepitia changamoto ya kunyanyaswa kijinsia unaweza kumsaidia kwa kumtengenezea mazingira ya yeye

Ku-open up kwako na kama itakua ngumu ni vizuri umshauri kuonana na mwanasaikolojia kwa ajili ya counseling.

Ni mbaya sana mtu anapopitia changamoto ya kunyanyaswa kijinsia kwa sababu anarudishwa nyuma sana kimawazo na kushidwa kuwa productive kama inavyompasa kuwa na baadhi yao vitendo hivyo huwapelekea kukatisha maisha yao, jambo ambalo linaacha majonzi kwa familia na jamii kwa ujumla.

kama tukiungana kwa pamoja tutakomesha kabisa vitendo hivi katika vyuo vyetu, usikae kimya unapofanyiwa au kuona mwenzako anapitia

changamoto ya unyanyasaji ni kupitia kuzungumza tu ndiyo tutakomesha kabisa vitendo hivi viovu.

Unyanyasaji wa kijinsia vyuo vikuu ni tatizo linalopaswa kupewa kipaumbele. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuunda mazingira ya vyuo vikuu yanayoheshimu haki za kila mwanafunzi na kusaidia katika kufanikisha malengo yao ya elimu na maendeleo.

Amini kwamba ‘sapoti’ yenu wakuu ndio kitu kinachofanya niendelee kupata nguvu thank you, wabeja sana until next time, ogopa matapeli kona ya wanavyuo ni moja tu “unicorner” until next time tchaoooooo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags