Kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu nchini Marekani ‘Universal Pictures’ imetoa tamko kuhusiana na minong’ono ya mashabiki kupitia mitandao ya kijamii ikidai kuwa mwanamuziki na mwigizaji Ariana Grande alilipwa pesa nyingi zaidi kuliko Cynthia Erivo katika filamu ya ‘Wicked’.
Kwa mujibu wa maoni ya watu katika mitandao ya kijamii ilieleza kuwa Grande ambaye aliigiza kwa jina la Glinda alilipwa kiasi cha dola milioni 15 huku kwa upande wa Erivo ambaye alicheza kama Elphaba alilipwa dola milioni 1 tu.
Kufuatiwa na malalamiko hayo kampuni hiyo imetoa ufafanuzi huku ikieleza kuwa nguli hao katika filamu ya ‘Wicked’ wote walilipwa fedha sawa.
“Taarifa za tofauti ya malipo kati ya Cynthia na Ariana si za kweli kabisa na zinatokana na uvumi wa mtandaoni. Wanawake hao walilipwa sawa kwa kazi yao kwenye filamu ya ‘Wicked,’” msemaji wa Universal Pictures alisema katika taarifa kwa chombo cha habari siku ya jana Novemba 26, 2024.
Utakumbuka kuwa filamu hiyo ilitoka rasmi Novemba 22, 2024 huku ikiwajumuisha waigizaji kama Jonathan Bailey, Ethan Slater, Michelle Yeoh, Jeff Goldblum na wengineo.
Leave a Reply