Unicomedy Tour kuanza Rasmi leo

Unicomedy Tour Kuanza Rasmi Leo

Ebwana eeeh!!! It's furahi day kama kawa kama dawa popote pale ulipo mwanafunzi wa chuo, hope uko poa kabisa.

Leo kwenye makala za burudani na michezo  utafahamu kuhusiana na kundi la Unicomedy Yaani University comedy.

Kama ilivyokawaida jarida la mwananchi scoop limepata wasaa wa kuzungumza kwa kina  na Mkurugenzi Mtendaji wa Unicomedy anayefahamika kwa majina Pascal Busenga maarufu kama Ganslay nakueleza mambo kadha wa kadha kuelekea tour hiyo.

Akizungumza na Mwandishi wa makala haya Ganslay alisema lengo la kuanzisha kundi hilo ni kukuza na kuboresha zaidi vipaji vya wanafunzi ambao wako vyuoni wenye malengo ya kufika mbali kupitia talanta zao.

Aidha alisema unicomedy ni platform ambayo inakutanisha wanafunzi walioko vyuoni ambao wanavipaji tofauti ikiwemo musician, fashion nk.

Hata hivyo ameelezea wazo la Unicomedy lilivyotokea  akidai kuwa ni idea ambayo wamekuja nayo kutokana na matakwa ya wanafunzi wenyewe kuhitaji kuwa na platform yao itakayowasaidia kuonyesha vipaji vyao.

Vile vile kwenye platform hiyo hakuna idadi maalum ya wachekeshaji kutokana  ni platform huru ambayo mwanafunzi yoyote mwenye kipaji ana uhuru wa kufanya kazi.

Sambamba na hayo ameweka wazi kuwa wengi wanaoperform kwenye unicomedy ni wanafunzi ambao wanatoka kwenye vyuo mbalimbali hapa nchini na wakichukua course tofauti.

“ Wengi wao wanatoka vyuo tofauti tofauti as I said  na wanasoma course tofaut kuna ambao wanatoka IFM, chuo cha maji, chuo cha Ardhi,Udsm, Dit, Tia, Dsj, Cbe, Mwalimu nyerere,  na vyuo vingine”alisema.

Aidha alielezea malengo ya tour hiyo ikiwemo ni kufanya matangazo na kuinfluence vijana kwa kuwafata vyuoni na kuwaelezea kuwa kuna Unicomedy.

“It’s all about production ambapo tunataka wanafunzi wa vyuo vyote waweze kuifahamu na wajue pia hii ni platform yao ili ijulikane zaidi tofauti na watu wengine wanavyoifahamu”alisema

Vile vile alisema mara nyingi Unicomedy hufanyika takribani mara tatu kwa mwaka ikiwemo mwezi wanne, mwezi wa sita na mwezi wa kumi na moja ambapo ikitokea fursa ya kupata sponsors inaweza kufanyika kila mwezi.

 “Actually tour zinatakiwa kufanyika two weeks before the main show lakini kama nilivyosema tunaifanya mara tatu kwa mwaka lakini kadri siku zinavyozidi kwenda tukipata sponsors tunauwezo wa kufanya kila mwezi”alisema.

Unaambiwa vita ni vita muraa lakini kwa upande wa unicomedy wao wanasema kuwa hawako kwa ajili ya kupambana na makundi mengine ya comedy kutokana na malengo ambayo wamejiwekea.

 “Most of comedians tunatokea cheka tu  wachache sana wanaotoka kwenye platform nyingine lakini asilimia 80 ya comedian wa uni comedy wanatokea cheka tu”alisema na kuongeza

 

“Hivyo hatuwezi kuchuana yaani kuweka ushindani saanaa kutokana na lengo letu sisi ni kuchekesha wanafunzi na kuenjoy na baada hapo  tunaenda kuchekesha watu wazima huko cheka tu hivyo hatuwezi kuchuana na ndiyomaana tunawaalika wasanii wengine kutoka kwenye hizo platform”alisema.

Hata hivyo Ganslay ametoa wito kwa wanafunzi walioko vyuoni akiwataka kutumia vipaji vyao vizuri na kuhakikisha wakipata fursa wanazitumia kadri wanavyoweza.

“Chuo ni good platform kwa wanafunzi yoyote Yule kujulikana hivyo ukitumia kipaji chako ukiwa chuoni tayari utakua unajenga future yako, hivyo tusibase tu darasani sana kwa sababu kuna fursa pia za kujiajiri hivyo lazima tuwe makini katika kuhakikisha tunayafikia malengo yetu hapo baadaye.”alisema

Aiseee ni wakati wako sasa ewe mwanafunzi uliopo chuoni kaa mkao wa kula kushuhudia event ya unicomedy itakayofanyika rasmi tarehe 20 november palee serena hotel kwa kushiriana na magazine ya Mwananchi scoop alwys be a scooper!!!!.
Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on Career and skills development every Monday and entertainment, every Friday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include SMARTPHONE and NIPE DILI.

Latest Post