Kwa watu wenye mahusiano au wanandoa kuachana ni jambo gumu sana katika maisha hususan kwa wanawake hasa ikiwa kwenye mahusiano hayo au ndoa hiyo kuna mtoto.
Ni jambo gumu kwa sababu kwa mwanamke atalazimika kuwa na mawasiliano na mwenza wake kwa muda mrefu mpaka pale mtoto atakapokuwa ametimiza miaka 18.
Kuna wakati kutakuwa na kutofautiana mara kwa mara jambo ambalo linaweza kusababisha msongo wa mawazo chuki na maumivu ya kihisia kwa mwanamke jambo ambalo linaweza kumchelewesha mwanamke kusonga mbele na maisha kwa kuwaza sana na kujuta kwamba labda mambo yangekuwa tofauti na siyo kuachana na mwenza wake aliyempenda sana.
Hata hivyo mitifuano kwenye mitandao ya kijamii ni jambo lingine linaloweza kuleta taharuki kwa wenza walioachana na kusababisha kuchukiana kusiko na sababu.
Ni vyema kama mwanaume ameamua kuvunja ndoa au mahusiano na kusonga mbele na maisha yake muache na huna haja ya kumlazimisha kukupenda wakati kwake yeye mapenzi yake kwako yameisha.
Kama yeye mwanaume ndiye tatizo achana naye na huna haja ya kujenga hasira na uadui dhidi yake kwa sababu hiyo haitakusaidia zaidi ya kukunyima usingizi, kuondoa furaha yako, kukufanya usiyafurahiye maisha na kukuletea maradhi ya kisukari na presha kwa sababu tu ya mtu ambaye huwezi kumbadili kuwa vile unavyotaka.
Kumbuka tu kwamba kumbeba mwanaume mlieachana naye kichwani ni kujisababishia maradhi yasiyo na lazima kwa sababu mapenzi ni hiyari na siyo lazima. Jambo muhimu kabisa ni kukubaliana na hali halisi na kusonga mbele na Maisha.
Vipi kama huyu mwanaume ataamua kuazisha mahusiano mapya, Je unaweza kuvumilia kumuona akiwa na furaha katika mahusiano hayo mapya?
Kama mwanamke upo mwanamume ambaye ndiyo ametoka kuachana na mwenzi wake na hataki kukubali kama ameachwa na kuanza visa na mitifuano katika mitandano ya kijamii, akikushutumu kwamba wewe ndiyo chanzo, je unawezaje kukabiliana na changamoto hiyo?
Leave a Reply