Baada ya kujuzana namna ya kupata wateja katika mitandao ya kijamii na jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kujipatia fursa, wiki hii Mwananchi Scoop imeangazia namna ambavyo unaweza kuepuka hasara katika biashara yako.
Siku zote wafanyabiashara tumaini lao kubwa ni kupata faida. Hivyo basi ili kufanikisha hilo ni muhimu kuzingatia mambo haya…
- Kuiga biashara
Ukiwa mtu unayetaka kufanya biashara na kupata faida acha kuiga, wekeza nguvu zako kwenye kuisoma biashara hiyo kuanzia faida, hasara, wateja nk, na ukishafanya hivyo utapata njia na miongozo ya namna gani ufanye, ili upate faida kuliko hasara.
- Kukosa uvumilivu
Hakuna biashara ambayo ukianzisha leo basi utaona faida kesho. Biashara zote lazima zipitie kwenye milima na mabonde hivyo basi unapoona biashara yako haiendi wala haupati fadia usikimbilie kuifunga unachotakiwa kukifanya, kuwa mvumilivu katika kila kipindi.
Wanasema anguko lako ndiyo tumaini/funzo lako. I hope ukipata changamoto basi itakujenga kiakili na baadaye kuja na mbinu mpya zenye kukupatia faida.
- Kuendekeza ndugu/rafiki
Jambo kubwa la kuogopa zaidi ni kuendekeza watu waliokuzunguka. Siku zote biashara inahitaji mtu aliyenyooka ambaye ataweza kuwazuia watu wanaomzunguka mfano familia, watoto, ndugu, marafiki wasiichukulia poa biashara yake.
Ukiwaendekeza watu hao kubali kuwa kupata faida kwako itakuwa changamoto. Ukiwa kama mfanyabiashara unatakiwa kuwa straight, serious na makini katika biashara yako.
- Kutoitangaza biashara yako
Usipoifanyia matangazo biashara yako basi utaishia kuitumia wewe na ndugu zako, ili uweze kuona faida basi unatakiwa kujitoa ufahamu na kuitangaza biashara yako katika mitandao ya kijamii. Unavyoitangaza ndiyo wateja wanavyozidi kuja na ndipo utaona faida yake.
Leave a Reply