Unapataje kazi bila kushikwa mkono

Unapataje kazi bila kushikwa mkono

Connection, conection, conection, nimeiita mara tatu waungwana, ni maatumaini yangu wote mnaelewa maana ya hili neno maana waswahili wanasema hata kazi ya kufagia barabarani inahitaji uwe na conection.

Na leo hapa tutadili haswa na wale waliomaliza vyuo na wenzangu na mie tunaotegemea connection ili kupata kazi.

Ngoja leo tuambizane ukweli hapa mpambanaji wangu. Je, ni kipi unafikiria baada ya kumaliza masomo yako? Je, kauli hii inatembea kichwani mwako au umeamua kujitambua na kufanya kile ambacho kinawezekana kulingana na wakati tulionao?

Katika karne hii ya 21 bado tuna vijana wanaamini kwamba baada ya kumaliza chuo na kufaulu ni ngumu kupata kazi mpaka ushikwe  mkono. Yaani atokee mtu akuwezeshe kupata ajira kwa kukupeleka mahali na kupewa kazi.

Haya ni mawazo mgando katika karne hii na kama bado unaota ndoto za namna hiyo basi utasubiri sana. Sikatai kwamba tunahitaji kupewa taarifa za maeneo ambayo yana ajira na taarifa hizo tunazipata kwa kutengeneza mawasiliano na watu mbalimbali kwenye mtandao wako hususani wale ambao wako kwenye ajira.

Lakini hiyo haimaanishi kwamba ndiyo ushikwe mkono na kupewa ajira kirahisi tu, haiwezekani.

Kama ikitokea umepata kazi kwa njia hiyo, basi wewe ni mwenye bahati na mtandao wako una nguvu sana una haki ya kudeka na kujivunia kuwa na ‘God Father’ wa kukuunganisha na fursa za ajira za namna hiyo.

Kama mwenzangu na miye ni pangu pakavu, ndugu yangu komaa mwenyewe kutafuta fursa za ajira kwa kuwania kila fursa unayoiona au unayopewa taarifa na mtandao wako bila kujali unamjua nani katika taasisi hiyo.

Mkumbuke tu kwamba wanaofanikiwa ni wale wenye uthubutu wa kuchangamkia fursa pale zinapojitokeza, Watu hawa huwa na positive attitude na kujiamini hata pale wanapo katishwa tamaa kwamba haiwezekani.

Tofauti na zamani, siku hizi mitandaoni ‘intaneti’ imerahisisha sana. Kuna mitandao inayotangaza nafasi za ajira mingi sana lakini pia makampuni mengi katika tovuti zao kuna kipengele cha ajira ambapo humo huwekwa nafasi za kazi zinapojitokeza lakini pia nyingine zinaruhusu muombaji kujisajili na kuweka taarifa zake hata kama hakuna ajira ili zikijitokeza wanakuita kwa usaili.

Kwa mfano, zipo kampuni kubwa za kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) za kimataifa huwa zinatoa fursa za ajira popote duniani katika maeneo waliyoweka matawi iwapo zinajitokeza nafasi za kazi.

Wenzetu wa nchi jirani wamechangamkia sana fursa hizo na ndiyo maana utawakuta popote utakapokwenda hapa duniani. Lakini vijana wetu ni waoga na hawana sifa ya uthubutu.

 Utakuta kijana muda wote saa 24 siku saba yuko kwenye mitandao ya Twitter, Facebook, Instagram akipiga soga lakini anashindwa kutumia muda wake kwenye mitandao ya ajira kutafuta kazi.

Lakini hata kujifunza zaidi kile alichosomea kupitia mitandaoni ya intaneti au kutafuta taarifa mbalimbali zinazohusiana na taaluma aliyosomea anashindwa na anajikita kwenye mijadala isiyo na tija.

Suala la kusubiri kushikwa mkono ili kupata fursa linawagusa pia wajasiriamali, nao kwa upande wao wakishaanzisha biashara  hawajiongezi kwa kupanua wigo wao wa masoko na badala yake wanategemea soko hilo hilo na hivyo wanajikuta mtaji hausogei so wewe kijana jua kujipambania mwenyewe usisubiri conection siku hizi hakuna kazi za kuunganishwa na mtu bali ni ujuzi wako.

Yees! hivyo basi kijana unatakiwa kujiamini na kuachana kabisa na misemo iliyopitwa na wakati kupata kazi ni wewe mwenyewe  namna utakavyoamua kujipambania katika maisha yako go-go-go my friend never say never.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags