Unalipa asilimia ngapi hili sanamu la Drake

Unalipa asilimia ngapi hili sanamu la Drake

Jumba la makumbusho maarufu la ‘Times Square’ kutoka New Yorka Marekani,  siku mbili zilizopita lilizindua sanamu la ‘rapa’ wa Canada Drake ambalo lilitengenezwa na Madame Tussauds kwa lengo la kumpa heshima msanii huyo.

Hata hivyo kupitia mtandao wa X (zamani twitter) baadhi ya mashabiki wametoa maoni kuhusu sanamu hilo ambapo baadhi yao walilisifia huku tatizo likiwa ni macho kuwa hayafanani na Drake, pia shabiki mwingine alifika mbali zaidi kwa kudai kuwa sanamu hilo ni bora zaidi kuliko la ‘rapa’ Lil Wayne.

Aidha katika maonesho hayo pia kulikuwa na baadhi ya sanamu za mastaa mbalimbali akiwemo Beyoncé, Dua Lipa, Megan Thee Stallion and Harry Styles na wengineo.

Kwa mujibu wa Tussauds ambaye ni mtengenezaji wa masanamu ya mastaa mbalimbali ameweka wazi kuwa yeye kufanya hivyo ni kwa ajili ya kuwatia nguvu wasanii hao kuendelea kuipeperusha bendera ya tasnia ya muziki Marekani.

Hii siyo mara ya kwanza Madame Tussauds kuchonga masanamu ya mastaa wa muziki Marekani Juni 15, mwaka huu alizindua sanamu la mwanamuziki Post Malone katika jukwaa la Governors Ball huko New York, na kumfanya ‘rapa’ Malone kufurahisha na kulikubali kwa silimia zote sanamu hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags