Miaka ya nyuma watu wengi walikuwa wakitumia makomeo ya kufunga na kufuli kwa ajili ya kulinda usalama wa mali zao za ndani, ingawa wapo wanaotumia hadi sasa lakini wengine wameenda mbali zaidi, huzitumia kufunga kwenye masanduku ya bati ya kuhifadhia vitu mashuleni.
Licha ya kuwepo kwa makampuni mengi ya kutengeneza kufuli, lakini yote huzitengeneza zikiwa na tundu dogo pembeni ya tundu la kuingizia funguo, wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiliona tundu hilo bila ya kufahamu sababu ya kuwekwa kwenye kufuli. hivyo basi fahamu kuwa tundu limewekwa kwa kazi yake maalumu.
Kutokana na mazingira ambayo kufuli hutumiwa kufunga nyumba wakati mwingine hupelekea kupata unyevu au kunyeshawa na mvua maji huingia ndani ya kufuli, hivyo basi tundu hilo dogo pembezoni mwa tundu la kuingiza funguo limewekwa kusaidia kutoa nje maji yatakayoingia kwenye kufuli.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply