Unaishije na watu wanaokatisha tamaa kazini

Unaishije na watu wanaokatisha tamaa kazini

Alooooh! It’ another Friday mtu wangu, kama kawaida yetu hatunaga mbambamba waswahili wanasema, sasa leo kwenye kazi na maisha nje ya kazi tumekuletea somo ambalo litakufanya usikate tamaa maisha yako yote.

Dunia ya leo imejaa maneno mengi kuliko watu na wingi wa maneno yaliopo ni ya kinafki. Hebu fikiria ya kwamba tafiti za wanasaikolojia zinasema ya kwamba, mwanaume huzungumza maneno 16,000 kwa siku, wakati wanawake wote duniani kwa kila mmoja mmoja huzungumza maneno 25,000 kwa siku, embu fikiria kwa tafiti hizo kutakuwa na maneno mangapi kwa kila mmja.

Najaribu tu kuwaza kwa sauti ili ujue ni kwa jinsi gani maneno yalivyozidi idadi ya watu. Nasema hayo kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukiishi katika ulimwengu wa kusema na kusikia. Na katika kusema wapo wale ambao huzungumza mambo chanya na wapo wale ambao huzungumza mambo hasi. Na katika kusikia ipo hivyo hivyo, sawa na kusema.

Na ukweli ni kwamba maneno ya watu ni sumu, maneno ya watu yana nguvu sana kuliko nguvu za Samson, hii ni kwa mujibu ya wahenga wapya. Uhalisia ulipo katika sayari hii ya kupeana taarifa, zimejaa taarifa za kukatishana tamaa kuliko kupeana mbinu za kusonga mbele kimaisha.

Na mara kadhaa hali hii hutokea na unaweza ukajikuta unaumia sana kwenye maisha yako, hivyo yote kwa sababu ya maoni hasi ya watu wanayokutolea wewe. Sasa ili usiendelee kuumia kwa jambo hilo, kumbuka hivi, hicho ambacho kinaongelewa juu yako ni kwa mujibu wa maoni yao wao wenyewe ila uhalisia wa wewe jinsi ulivyo unaujua wewe. 

Hivyo, tunachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba, acha kuchukua maoni ya watu na ukaamua kuyatumia kuendesha maisha yako, kwa sababu kama ukifanya hivyo utaumia sana na utaiona dunia chungu.  Hivyo ni vyema ukaamua kuishi wewe kama wewe kwa kufata yafuatayo:

>Usipende kumshirikisha kila mtu mambo yako

>Punguza mazoea na watu kazini ili kuepukana na maneno maneno

>Punguza marafiki ambao hawa ni wanafiki kwa upande wako, sio lazima kila mtu awe rafiki yako

> Usipende kuweka mambo yako katika mitandao ya kijamii

> Ishi maisha yako ili kuepukana na maneno ya kukatisha tamaa. Inabidi kuishi maisha yako usimuige msanii yoyote wala mtu yoyote kazini kwamba akifanya jambo fulani nawewe lazima ufanye 

Oyeea! Wanangu wa Mwananchi Scoop tumalizie kwa kusema ya kwamba, endapo utaamua kufanya maamuzi sahihi pasipo kuwasiliza wakatishaji tamaa katika dunia hii, kutakufanya uishi maisha ya ushindi siku zote za Maisha yako.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post