Unaikumbuka ‘Zeze’ na ‘Siamini’ ya Tid

Unaikumbuka ‘Zeze’ na ‘Siamini’ ya Tid

Ni mwanamuziki wa Tanzania ambaye jina lake kamili ni Khalid Mohamed huyu si mwingine ni msanii wa bongo fleva maarufu kama TID.

TID ina maana ya 'Top In Dar es Salaam' mjini anakoishi.

Eee bwana msanii huyu tunampenda na ndio maana leo katika TBT tumekusogezea nyimbo zake zote mbili ambayo ni 'Zeze' na 'siamini'.

Unaambiwa kuwa TID alianza kuimba mwaka 1994 na kundi kwa jina Black Gangsters.

Alianza kuimba pekee miaka mitano baadaye akiwa na umri wa miaka 21 baada ya kuandikisha mkataba na Poa Records.

Hata hivyo wimbo wake wa kwanza ulijulikana kwa jina la 'Mrembo' ulitolewa 2002 lakini haujawahi kuvuma kama wa Zeze na Siamini.

Mbali ya kuimba, TID aliwahi kuigiza katika filamu ya Girlfriend, hakika filamu hiyo ilipendwa na watanzania wengi kutokana na walioigiza kuvaa uhusika wa kweli.

Basi msomaji wetu kama una comment juu ya hichi tunachokuhabarisha usisite kutujuza ili tuweze kufanyia kazi yale yote tunayoyakosea.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags