Unaijua kazi ya mfuko mdogo kwenye suruali ya Jeans

Unaijua kazi ya mfuko mdogo kwenye suruali ya Jeans

Suruali ya jeans ni kati ya vazi linalopendwa sana mtaani, lakini kama umewahi kulichunguza vazi hili lazima utakuwa umekutana na kifuko kidogo kilichopo juu ya mfuko mkubwa, wapo baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kazi ya kifuko hicho bila ya kupata majibu.

Toleo la kwanza la suruali ya jeans yenye mifuko miwili yaani mdogo na mkubwa liliingia sokoni mwaka 1870s ikitengenezwa na ‘Levi Strauss’.

Huku kazi ya kwanza ya mfuko huo ikitajwa kuwa ilikuwa ni mahala salama pakuhifadhia saa kutokana na kipindi hicho hakukuwa na saa za mikanda za kuvaa mkononi, bali kulikuwa na saa za mfukoni ambazo zilitamba sana na zilikuwa za bei rahisi zilizokuwa zikitambulika kwa jina la ‘Charles Hubert pocket watch’.

Lakini kwa miaka ya hivi karibuni mfuko huo umeonekana kama urembo katika Suruali, na kwa baadhi ya watu wanatumia mfuko huo kuhifadhia vitu ambavyo ni rahisi kupotea kama vile sarafu, funguo, na tiketi za daladala.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post