Unafahamu nini kuhusu akili bandia (AI)

Unafahamu nini kuhusu akili bandia (AI)

Inawezekana hivi karibuni ukawa umesikia sana kuhusu kitu kinachoitwa AI kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye ofisi, mitaani na hata kwenye mitandao ya kijamii.

Swali kubwa unalojiuliza ni nini kitu hicho? leo naomba nikujuze zaidi ili uwe na elewa mpana kuhusu Hili.

AI ni kifupi cha "Inteligensia Bandia” (kwa Kiingereza, Artificial Intelligence).

Hii ni eneo la sayansi ya kompyuta linalohusika na maendeleo ya programu na mifumo inayoweza kufanya kazi kama akili ya binadamu.

Lengo kuu la AI ni kuunda programu au mashine zenye uwezo wa kufikiri, kujifunza, na kufanya uamuzi kama binadamu.

Kuna aina mbalimbali za AI, ikiwa ni; AI ya Kufikiria (Symbolic AI) ambayo hujumuisha matumizi ya mantiki na alama kwa ajili ya kufikiri na kutoa uamuzi.

Ya pili ni Machine Learning (Kujifunza Mashine) yenyewe Inahusisha programu kujifunza kutoka kwa data na kuboresha utendaji wake bila kuwa na programu maalumu.

Ya tatu ikiwa ni Deep Learning (Kujifunza Kina) ambayo ni sehemu ya kujifunza mashine inayotumia mitandao ya neva kufanya uchambuzi wa data na kujifunza.

AI inatumika katika maeneo mengi kama vile lugha asilia, taswira, michezo ya kompyuta, utambuzi wa sauti, magari yasiyo na dereva, na zaidi.

Kimsingi ni uwanja unaokua kwa kasi na una mchango mkubwa katika teknolojia na maendeleo ya viwanda mbalimbali.

 

Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii hasa Instagram kuliibuka

mjadala kuhusiana na mrembo aliyefahamika kwa jina la Emily Pellegrini ambaye amekuwa akiachia picha zenye kuvutia zikionyesha baadhi ya maungo kwenye mwili wake.

Cha  kushangaza zaidi kinatajwa kuwa yeye si mwanadamu halisi bali ni AI imetumika kumtengeneza.

Jambo hilo liliteka hisia za watu wengi kwenye mtandao huo na kuanza kuhoji je ni kwa namna gani kitu kama hicho kimefanyika.

Mmiliki na mwendeshaji wa ukurasa huo wa instagram aliamua kuweka wazi baada ya kuona kuwa ukurasa wa mrembo huyo ukifuatiliwa na watu mashuhuri na matajiri wakimuhitaji kuwa na urafiki naye kutokana na urembo wake ambao haukuwa na uhalisia wowote.

Lakini si picha au video za watu tu zinaweza kutengenezwa kupitia teknolojia hii bali hata mifumo ya uendeshaji kwenye utoaji huduma bandia.

 Hivyo inaweza kusababisha watu kutapeliwa kwa njia moja ama nyingine hivyo ni vyema kuwa makini kwenye eneo hili.

 

Na Ammari Masimba

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post