Ukitaka kusuka kibali million 1, Zanzibar

Ukitaka kusuka kibali million 1, Zanzibar

Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar Dkt. Omar amesema Askari wake wameanza kukamata Wanaume wote wanaosuka nywele kama za Wasichana wakiwa Zanzibar bila kibali maalum na kusema iwapo Mwanaume atataka kuwa na kibali cha kusuka atatakiwa kulipia shilingi milioni 1.

Dkt. Omar Adam amesema hayo leo kwenye Asubuhi Njema ya ZBC wakati akieleza mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Sanaa na Filamu na namna wanavyosimamia Mila, Desturi na Utamaduni wa Zanzibar.

“Askari wanakamata Wanaume wote wanaosuka nywele kama za Wasichana, Baraza la Sanaa hatupendelei hilo na kuna kibali maalumu cha kusuka nywele ambacho ni milioni 1 na tumeweka bei hiyo ili kuwakomoa, sasa utachagua mwenyewe utoe milioni usuke au ununue kiwembe chako unyoe” amesema Dr. Omar.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags