Ukitaka kunukia kama Beyonce uturi laki nne

Ukitaka kunukia kama Beyonce uturi laki nne

Baada ya kutoa taarifa katika ziara yake ya Renaissance kuhusiana na uzinduzi wa Perfume yake, hatimaye mfanyabiashara na mwanamuziki Beyonce amezindua manukato hayo ambayo yanapatikana kwa kutoa ‘oda’.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Beyonce ame-share promo ya perfume hiyo huku akieleza kuwa manukato hayo yataanza kuingia sokoni Novemba kwa oda.

Manukato hayo yaliyopewa jina la CE NOIR yanapatikana kwa ‘oda’ kwenye tovuti ya mwanamuziki huyo huku bei ya uturi huo ikiwa ni $160 ambapo ni sawa na zaidi ya laki nne za Kitanzania ambapo inadaiwa kuwa manukato hayo yatauzwa Marekani na Canada pekee.

Miezi kadhaa iliyopita Beyonce na binti yake Blue Ivy walishika vichwa vya habari baada ya kuupiga mwingi katika ziara yao waliyoipa jina la ‘Renaissance World Tour’ iliyoanza May na kutamatika Oktoba 1 mwaka huu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags