Ukigundua mwenza wako ana ujauzito fanya mambo haya

Ukigundua Mwenza Wako Ana Ujauzito Fanya Mambo Haya

Aiseeee nikukumbushe tu masuala machache ambayo unaweza kuyafanya mara tu utakapogundua kuwa mwenza wako anaujauzito basi hakikisha unapita kwa uaminifu mkubwa sana kwenye njia hizi.

Njia ziko nyingi sana mdau wangu lakini tumekuwekea hizo chache ambazo ukizifuata basi hutokuja kujuta hapo baadae baada ya mwenza wako kujifungua fuatilia dondoo hii kwa umakini utajifunza jambo.

Pindi utakapogundua kuwa anaujauzito basi  anzeni kuweka akiba kulingana na uwezo wenu hasa robo ya mnachozalisha. Ni lazima kujiandaa kiuchumi ili Mtoto akifika usipate shida.

 Kama mnaishi pamoja, ujauzito  ukishafikisha siku 120 (Miezi Minne) anzeni kuomba pamoja na Mtoto aliye Tumboni, mkimuombea mema kwa kutamka maneno kadiri ya namna mnavyotaka Mtoto awe

 Mjamzito azingatie Vyakula vyote vyenye virutubisho ikiwemo Mbogamboga, Matunda, Vyakula vya Protini na Wanga. Kama una kipato kidogo anza kununua vitu vya Mtoto taratibu usisubiri mpaka Mama ajifungue

 Mwepushe Mjamzito na Mazingira hatarishi kama kulala bila chandarua, Kula vyakula ovyo mtaani au kunywa maji yasiyo salama kama hayakuchemshwa nk.

Ahsantee bila shaka ni darasa fupi sana lakini linamanufaa makubwa kama ukizingatia hayo kwa uchache  wake unaweza pia kujiongeza kwa mengine unayoyafahamu.

 


Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post