Ugiriki kumtemea mate mtu ni baraka

Ugiriki kumtemea mate mtu ni baraka

Na Asma Hamis

Bongo ukimtemea mate mtu kama sio ugomvi wa kurushiana maneno basi ngumi zitalika. Lakini nchini Ugiriki jambo hilo ni kawaida huku wakiliita baraka.

Ugiriki wanaamini kumtemea mate mtu mara tatu huku ukitamka maneno haya ‘Ftou Ftou Ftou’ ni ishara ya bahati nzuri na kinga dhidi jicho baya (hassad au husda).

Tukio hili la kutemeana mate hufanyika katika sehemu mbalimbali ikiwemo wakati wa shughuli ya harusi au ndoa, wageni waalikwa watatakiwa kuwatemea mate maharusi kama ishara ya kufukuza roho chafu na kuwapa baraka maharusi hao katika ndoa yao mpya.

Mbali na sehemu hiyo pia jamii ya Ugiriki inaamini kuwa unaposikia mtu anazungumza kuhusu shida au matatizo basi utatakiwa kumtemea mate huku ukisema ‘Ftou Ftou Ftou’ kufanya hivyo kutasaidia kuepuka shida na matatizo.

Vilevile wavuvi hutemea mate kwenye nyavu zao, ili kuhakikisha wanapata samaki wengi na watoto wa Kigiriki wanatemewa mate huku wazazi wakisema “Ftou Ftou Ftou” kila wakati ili kumfukuza shetani.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa jambo hilo linaaminika kuwa na sifa ya utakaso kila wakati tema mate mara tatu na utakuwa salama kutoka kwa jicho baya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags