Serikali ya Uganda inapanga kuongeza umri wa unywaji pombe kutoka miaka 18 hadi 21 ili kukabiliana na uraibu, afisa wa Wizara ya Afya ameeleza.
Akizungumza katika Kongamano la Pili la Wakuu wa Kitaifa 2023, tukio lililolenga kuandaa hatua za kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kwa wanafunzi nchini Uganda, Kamishna wa Wizara ya Afya ya Afya ya Akili, Pombe na Madawa ya Kulevya, Dk Hafsa Lukwata alisema “Tunataka kupunguza idadi hiyo ya watu ambao watanunua, tunataka kuongeza umri kutoka 18 hadi 21”
Kulingana na hayo, sayansi imeonyesha kwamba ikiwa mtu hajatumia dawa za kulevya kufikia umri wa miaka 21, nafasi za kuwa mraibu baadaye katika maisha yao hupungua.
Ripoti ya 2023 iliyotolewa na shirika la afya duniani, kwa wastani, raia wa Uganda hutumia lita 12.21 za pombe safi kila mwaka. Wanaume hutumia zaidi ya wanawake, na wastani wa lita 19.93 za pombe safi kila mwaka ikilinganishwa na lita 4.88 kwa wanawake.
Aidha hivi punde Shirika la Afya Duniani (WHO) imeiweka Uganda nafasi ya kwanza katika matumizi ya pombe katika bara la Afrika.
Leave a Reply