Ufahamu mtindo wa ‘Iro na Buba’ unavyobamba kwa wanawake

Ufahamu mtindo wa ‘Iro na Buba’ unavyobamba kwa wanawake

Eiwaaaah!! Mambo vipi? wapenzi wa fashion na wafuatiliaji wa magazine ya Mwananchi scoop kama ilivyo kawaida yetu hatujawahi kukuacha mtupu bwana.

Ebwana eeh hivi umewahi kuusikia ama kuona mtindo huu unaofahamika kama Iron a Buba?kama bado na ni mgeni kwenye upeo wa masikio na macho niko tayari kukujuza hapa.

Leo kwenye kipengele cha fashion tutaangazia mtindo huo ambao umebamba sana hususani kwa wanawake na umejizoelea umaarufu mkubwa karibu kufuatilia dondoo hii.

Je unafahamu mtindo wa mavazi wa ‘Iro and Buba’ ni moja kati ya mtindo unaoweza kukupa muonekano bomba na kwa gharama nafuu?

Si hivyo tu, mtindo huo ndiyo habari ya mjini kwa sasa na unaweza kuvaliwa katika matukio mbalimbali ikiwemo harusi, sendoff, kitchen part na hata katika mitoko mingine.

‘Iro and Buba’ iro inakuwa ni aina ya sketi ya kufunga na buba ni aina ya blouzi ambayo ni pana na hutumika kuvalia na sketi hiyo.

Halima Abdalah mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam alisema anapendelea sana mtindo huo kutokana na kuwa hauihitaji mambo mengi hivyo kumuwezesha kupata muonekano wa kisasa kwa gharama nafuu.

“Tofauti na mitindo mingine ambayo itakuhitaji kuwa na vitambaa vya kuchanganyia, lace material na mambo mengine ili kupata muonekano bomba wa kwenda katika shughuli mbalimbali ikiwemo harusi, pia haitumii muda mwingi katika kushona kutokana na aina ya sketi ambayo ni ya kufunga,”alisema.

Kauli hiyo inaenda sambamba na Abdul Kilumbi anayejishughulisha na ushonaji wa mavazi ya kike na kiume kutoka Kilumbi Fashion anaeleza kuwa kama akitulia na kushona nguo ya mtindo huo pekee anaweza kutumia chini ya saa 2 kushona.

Alisema ni aina ya mtindo ambayo inaweza kuvaliwa na mwanamke wa aina yeyote na akapendeza cha msingi ni kujua kufunga vizuri sketi kwani hapo ndipo msingi haswa wa mtindo huo wa mavazi ulioshika kasi miezi ya hivi karibuni.

“Mtindo huu si mpya katika ulimwengu wa fashion huwa unakuja na kupotea lakini kila unapoibuka tena huja ukiwa umeboreshwa haswa katika ufungaji wa sketi,”anasema.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali za masuala ya mitindo, Asili ya mtindo huu ni nchini Nigeria ambalo huwa linavaliwa sana na wanawake wa kabila la Yoruba linalopatikana maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

Wayoruba ni kabila la pili kwa ukubwa nchini Nigeria ambalo linafahamika kwa kupenda sherehe za shamrashamra nyingi na sherehe za kila wakati.

Aina hii ya mavazi ilianza kushika kasi mnamo miaka ya 1950 hadi mwanzo mwa miaka ya 1980 na kwa mujibu wa tovuti mbalimbali za mitindo nchini humo mavazi haya yalikuwa yakivaliwa na wanawake sana na wanawake wenye umri mkubwa na lilikuwa maalum kwa ajili ya kuvaa harusini.

Alooooh! Bilashaka utakua umepata ufahamu mkubwa juu ya vazi hilo kwa taarifa na mitindo mbalimbali kwenye anga za fashion usikose kufauatilia magazine ya Mwananchi scoop.

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post