Ufahamu mgahawa wa kutisha, wahudumu kama mazombi, chakula laki 5

Ufahamu mgahawa wa kutisha, wahudumu kama mazombi, chakula laki 5

Aliyesema kuishi kwingi kuona mengi wala hakukosea, kama unahisi umeona kila kitu hakika utakuwa unajidanganya kwa sababu ya dunia ni mengi na yanazidi kuongezeka kila kukicha.

Waliyo wengi hasa wapenzi wa movie neno 'Zombie' si geni masikioni na machoni mwao, kutokana na kutazama filamu mbalimbali zinazoenesha viumbe hao wakutisha. Fikiria kama kweli siku utakutana na viumbe wa aina hiyo itakuwaje?



Wakati ukiendelea kufikiri fahamu kuwa kuna mgahawa mmoja nchini Malaysia ambao wahudumu wake huvalia mavazi na vinyago vya ‘mazombi’ ili kuwa na muonekano wa kutisha wakati wa kutoa huduma ya chakula kwa wateja na mazingira ya mgahawa huo ni yakutisha.
Mgahawa huo unafahamika kwa jina la ‘Bunian The Haunted Café’, ambao mwanzo wanandoa Rohzairee Zainal na Aqilah Faqihah , walinunua eneo hilo la duka bila kuwa na wazo lolote la wanachofanya sasa.

Lakini walikuja kugundua kuwa eneo hilo lipo karibu na Makumbusho ya Historia ya Mizimu, linalofahamika kama ‘Ghost Museum Melaka’.


Ndipo baada ya kugundua hilo iliwabidi kufungua mgahawa huo ambao wafanyakazi wake wamekuwa na ubunifu wa mavazi na aina ya kuhudumia, hasa kuwa na muonekano wa kutisha ili kuendana na historia ya eneo walilopo.


Pamoja na kuvalia vitu vya kutisha lakini pia katika eneo la mgahawa huo kumekuwa na mishumaa na picha mbalimbali za kutisha huku aina ya muziki wa taratibu unaopigwa eneo hilo huwa na sauti za kutisha.


Hata hivyo vyakula vyao hupikwa kawaida kabisa, bila kuwa na muonekano wa kutisha, ambavyo vinaweza kuliwa na mtu yeyote.
Kutokana na muonekano wa kila kitu katika eneo hilo imekuwa kivutio ambacho watu wengi huvutiwa na kwenda kupata chakula huku wakiogopa.


Wamiliki wa mgahawa huo wanaeleza kuwa si watu wa eneo hilo tu, wanaoenda kununua chakula, bali wapo watu wanaofunga safari kutoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kula na kuona vitio cha eneo hilo.

Inasemekana bei ya chakula katika eneo hilo ni zaidi ya laki tsh 500k.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags