Uchaguzi wa mambo juu ya maisha yetu

Uchaguzi wa mambo juu ya maisha yetu

Kijana mwenzangu nafahamu kuwa mara nyingi katika maisha yako uwa vipo vitu ambavyo ukivielewa na kuvifanyia kazi vizuri  vinauwezo mkubwa wa kubadilisha maisha yako na kukuletea mafanikio makubwa unayoyataka.

Pamoja na kuwa vipo vitu vingi ambavyo vinauwezo mkubwa wakubadilisha maisha yako, lakini leo katika Karia hapa nataka kukushirikisha kitu kimoja tu pekee wewe kijana ambacho kina nguvu ya kubadilisha yako na yakawa ya tofauti kabisa.

Kitu hichi nitakachokueleza ndicho ambacho kwa sehemu kubwa kinauwezo wa kukufanya ukawa mtu wa mafanikio siku zote au wa kushindwa, pia kitakufanya uwe na fedha au ukose kabisa fedha.

Hata hivyo kutokana na wengi kutokukielewa ama kukitambua kumesababisha kuishi maisha magumu na ya mateso siku zote.

Kitu hiki ambacho nataka kijana mwenzangu hasa uliyopo chuoni ukijue si kingine bali ni Uchaguzi unaoufanya kila siku juu ya maisha yako.

Ili uweze kunielewa vizuri, hebu kumbuka kitu hiki. Watu wote duniani haijalishi rangi, dini, kabila au taifa wote tulikuja hapa duniani tukiwa tupu, nikiwa na maana tukiwa hatuna kitu, tulikuja kama tulivyo sisi.

Ni kitu gani ambacho kilikuja kubadili maisha na kuyaona kama yalivyo sasa hivi wengine wakiwa maskini na wengine wakiwa matajiri, ni uchaguzi tunaoufanya juu ya maisha yetu ya kila siku.

 

Uchaguzi huu wa mambo ni jambo la msingi sana katika maisha yetu kwani yanaleta mabadiliko na hapa nitakuuliza kuwa kwa nini usichague kuishi maisha unayotaka kuishi, badala ya kukaa tu na kuamuliwa na mazingira ambayo yanaweza kukupeleka kokote kule?

Kwanini uendelee kulaumu kila siku maisha ni magumu, sinafedha, sina kile wala kile na kuumia tu bure? Kaa chini na ufanye uamuzi wamaana juu ya maisha yako leo unataka yaweje.

Ukweli ni kwamba wewe ndiye unayeamua maisha yako unatakayaweje.

Wewe ndiye unayechagua na sio mtu mwingine. Tabia ulizonazo ni uchaguzi wako, kufikiri kwa namna fulani, kutafsiri kwa namna fulani matukio yanayokukuta maishani mwako, vyote niuchaguzi wako.

Unaweza ukasingizia mazingira na hali mbalimbali, kwamba ndivyo vimekufanya uwe hivyo kama ulivyo, lakini ukweli unabaki palepale, wewe ndiye unayechagua maisha yako yawe vipi.

Kumbuka siku zote kuwa kufanikiwa au kutokufanikiwa maishani ni suala la uamuzi wako mwenyewe, kama vile unavyoamua kuoga au kutooga asubuhi kabla hujatoka nyumbani kuelekea kazini kwako na mafanikio yapo hivyohivyo.

Ninaposema ni suala la uamuzi si maanishi uamue leo kufanikiwa na kesho uwe tajiri, hapana. Mafanikio yanakutaka wewe uanze kuweka mipango na malengo kwanza na kisha kuitekeleza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags