Uchafu wa kwenye simu umezidi wa chooni

Uchafu wa kwenye simu umezidi wa chooni

Imekuwa kawaida kwa baadhi ya watu kuwa karibu na simu zao za mkononi kila mahali waendapo, na inaelezwa kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watu duniani wanamiliki au kutumia simu janja wengi wao hawawezi kakaa mbali na vifaa hivyo vya mawasiliano.

Utafiti wa mwaka 2019 uligundua kuwa asilimia 74.5 ya watu nchini Marekani hutumia simu zao wakiwa chooni hivyo basi tafiti zimegundua kuwa simu ni chafu kuliko vyoo vyenyewe.

Mbali na tafiti hiyo kama ilivyozoeleka katika maeneo mengi aendayo mtu huwa na simu yake hivyo simu hupokea bakteri na virusi mbalimbali vya magonjwa kutoka kwenye maeneo zilipowekwa na kwenye mikono ya mmiliki endapo akishika kitu kichafu na kuishika simu yake bila ya kunawa.

Hivyo ni wazi kwamba kuna umuhimu wa kusafisha simu mara kwa mara sababu virusi vinauwezo wa kuishi kwa siku kadhaa sehemu ngumu na plastiki. Ni vizuri kutumia wipes zilizo na 'sanitaiza' au dawa, baada ya kumaliza kusafisha simu ni muhimu kuosha mikono vizuri kwa maji na sabuni.

Aidha muhimu kuweka simu yako mfukoni au kwenye begi wakati hauitumii na siyo kuiweka kila mahali, epuka kushiriki simu yako na watu wengine na ukifanya hivyo hakikisha unaisafisha, pia usafi huo unaenda sambamba na kwa chaja ya simu yako.

Ni hatari kiafya kuwapa watoto simu kabla ya kusafisha kwani baadhi yao hupenda kuziweka mdomoni kwa watu wazima pia si vizuri kutumia simu wakati wa kula chakula kwani inaweza kuwa sababu ya kuamisha vimelea vya bakteria na kuviweka mdomoni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags