Tyson atarajia kupata mtoto wa nane

Tyson atarajia kupata mtoto wa nane

Bondia maarufu kutoka nchini Uingereza #TysonFury, ameweka wazi kuwa anatarajia kupata mtoto wa nane na mkewe #ParisFury.

Fury ameweka wazi suala hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya ku-posti picha ya mkewe huku akimwagia sifa kwa kudai kuwa licha ya kuzaa naye watoto saba lakini bado mkewe huyo ni mrembo.

Hata hivyo bondia huyo wa ngumi za kulipwa amesema kuwa yeye na mkewe hawatoishia watoto hao kwani wanampango wa kuwa na familia ya watoto kumi.

Fury na Paris wamekuwa katika ndoa kwa kipindi cha miaka 15 ambapo mpaka kufikia sasa wamebahatika kupata watoto saba.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags