Tyrese kuburuzwa mahakamani na Ex wake

Tyrese kuburuzwa mahakamani na Ex wake

Mke wa zamani wa mwigizaji Tyrese Gibson, Norma Mitchell amemshitaki Ex wake huyo baada ya kudai kuwa Tyrese alimchafua kwa kuposti habari binafsi kuhusu yeye pamoja na binti yao Shayla (16).

Kesi dhidi ya mwigizaji huyo ilifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Kaunti ya Los Angeles Marekani, siku ya Jumanne, Mei 7 ambapo Mitchell alidai kuwa amekashifiwa na Tyrese kupitia posti alizoshare katika ukurasa wake wa Instagram kati ya Aprili 30 hadi Mei 7 mwaka huu ambapo alidai kuwa machapisho hayo yameharibu Cv yake.

Hayo yote yanakuja baada ya Tyrese miezi kadhaa iliyopita kuwasilisha ombi katika mahakama ya familia akidai malezi ya mtoto wake huku akiamini kuwa mkewe huyo wa zamani hana uwezo wala fedha za kumsomesha binti yao.

Mkali huyo wa 'Fast and Furious' na Norma Mitchell waliofunga ndoa mwaka 2007 na kutengana 2009 ambapo walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Shayla.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Tyrese kukutwa na kesi za aina hii mwaka 2023 alishitakiwa na aliyekuwa mke wake wa pili Samantha Lee aliyefunga naye ndoa 2017 na kuachana 2020 kwa kuharibu nyumba aliyokuwa akiishi Lee iliyoko Woodland Hills.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post