Tyrese amkumbuka Paul Walker

Tyrese amkumbuka Paul Walker

Mwigizaji na mwanamuziki wa R&B kutoka nchini Marekani Tyrese Gibson ameoneka kumkumbuka sana marehemu mwigizaji Paul Walker, hii ni baada ya kuangua kilio wakati alipoliona gari la mwigizaji huyo aina ya ‘Nissan Skyline’ alilolitumia kwenye ‘Fast and Furious’ 2.

Kupitia video inayosambaa mitandaoni ilimuonesha akitokwa na machozi baada ya kuliona gari hilo kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi ambapo ndinga hiyo imeendelea kusalia katika moja ya ‘yadi’ za magari nchini humo ikiwa kama alama ya kumuenzi na kumkumbuka Walker.

Ikumbukwe kuwa nyota wa filamu ya ‘Fast and Furious’ Paul Walker (40) alifariki pamoja na rafiki yake Roger W. Rodas Novemba 30, mwaka 2013 baada ya kupata ajari ya gari Los Angeles nchini Marekani.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post